Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili
katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Alhaj Ali Hassan
Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) aliowaita leo
nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam,wakati alipozungumzia
swala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa
kipindi cha hivi karibuni.Mzee Mwinyi ametoa rai kuwa Swala hilo ambalo
limekuwa na utata mkubwa na kupelekea kuzua vurugu kwa baadhi ya maeneo
hapa nchini,kuwa liachiwe watu wenye dharula kama linavyoelekeza kwenye
Moja ya Vitabu vya dini.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wamsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu,Alhaj Ali Hassan
Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya waandishi wa Habari
waliofika nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment