Baba
wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa
Tanganyika na zanzibar kuashiria Muungano wa nchi hizi mbili mnamo
aprili 26 mwaka 1964
Ndugu Wa Tanzania,
Kwa
niaba ya tawi la Chama Cha Mapinduzi Uingerez,na kwa niaba yangu
binafsi, Napenda kutoa salamu kwa Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho
Kikwete, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.
Ali Mohammed Shein kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na
kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka 49 ya Muungano wa nchi
yetu, TANZANIA.
Pamoja
na salamu hizo, binafsi na kwa niaba ya wana CCM UK ,napenda kuwaomba
na kuwakumbusha WaTanzania wenzangu, tuendelee kuuenzi na kuulinda
Muungano wetu kwa kudumisha AMANI, UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO.
Hizi ndizo silaha zilizoweza kuulinda Muungano huu ambao umetuletea
Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa nusu karne sasa.
Ndugu
Wa Tanzania, nawasihi kamwe tusichezee amani tuliyonayo. Tujifunze
kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo
ndani ya dimbwi kubwa la machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea
kila kukicha
Aidha,
Watanzania wa Nje ya Nchi (Diaspora)tunajivunia na kutambua kwamba tuna
nafasi ya pekee ya kuchangia katika maendeleo ya Nchi yetu Tanzania
katika Nyanja tofauti . Mojawapo ya Mchango wetu Mkubwa kwa Taifa ni
kufuatilia kwa ukaribu mambo yanayoendelea nyumbani ,na kutoa mchango
wetu wa kimawazo pale inapobidi.
CCM-UK
tutaendelea kutoa shukrani za dhati kwa Mwenyekitiwa CCM Taifa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete , pamoja na
Serikali yake anayoiongoza kwa kuona umuhimu wa kutushirikisha Wana
Diaspora na kuthamini mchango wetu.
Tunafarijika
sana na kuahidi siku zote kwamba tutaendelea kuchangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya Tanzania, kama inavyowezekana kwa raia wengine
Wengi
Ulimwenguni wanaoishi nje ya Nchi zao na wana changia kukuza uchumi na
kuendeleza jamii zao kwa kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza
ughaibuni.
Mwisho nawatakieni watanzania wenzangu kusherehekea sikukuu ya muungano kwa amani na Utulivu mkubwa.
Tuwaenzi waasisi wetu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuulinda muungano.
MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, SI NDOTO YANAWEZEKANA.
Kwan niaba ya CCM UK – Nawatakia Watanzania wote popote pale walipo Duniani Maadhimisho na Sherehe njema za siku hii adhimu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA – MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
—————————————————–
Mariam A. Mungula
KATIBU
CHAMA CHA MAPINDUZI – UINGEREZA
No comments:
Post a Comment