Barabara mpya inayojengwa kuunganisha kata ya Tegetero na kibongwa morogoro kusini ili kurahisisha usafiri kati ya kata hizo.
Barabara hiyo itakapokamilika itakuwa na urefu wa kilometa 15 itapitia katika kijiji cha tegetero na Halmashauri ya morogoro vijijini wametenga jumla ya shilingi milioni 35 na mbunge wa morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris amejitolea greda linalofanya ujenzi huo pia kugaramia mafuta ya kuendesha greda hilo wakati wote wa ujenzi,
Mdau wa maendeleo wa morogoro kusini aliyeambatana na mbunge huyo akikatiza katika barabara hiyo wakati ujenzi huo unaendelea.
Ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea na viongozi wa serikali za vijiji na mitaa wakiwa eneo la tukio kusaidiana na mbunge huyo katika kutekeleza ujenzi huo,Viongozi hao wa vijiji wanasaidiana katika hali na mali kufanikisha ujenzi huo
tunatamani barabara ya morogoro kisaki na msalabani Lanzi (nyingwa) ikamilike. vipi kuhusu umeme?
ReplyDelete