Jengo la Kituo cha Afya linalojengwa katika kijiji cha tawa morogoro kusiniUjenzi wa jengo hili utasaidia kupunguza tatizo la wananchi wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya hususani afya ya mama na mtoto katika jimbo la morogoro kusini.
Mradi wa ujenzi wa kituo hiki cha afya utagarimu jumla ya shilingi billioni 1.4 mpaka utakapokamilika ambapo gharama hizo ni pamoja na jengo na mfumo wa nishati ya umeme wa jua ambao unafadhiliwa na watu wa austria.
Mradi huu utakapokamilika utawezesha pia kituo hiki kufanya oparesheni hali ambayo itasaidia sana kutatua tatizo sugu za afya katika jimbo la morogoro kusini linaloongozwa na mbunge Mh Innocent Kalogeris
Mbunge wa morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris mbele akiwa ametoka kukagua maendeleo ya ujenzi huo juzi wakatia akiwa katika ziara ya kuwatembelwa wqananchi wake pamoja na kukagua miradi inayoendelea jimbo la morogoro kusini wilaya ya morogoro vijijini
No comments:
Post a Comment