IMG_1567
Picha juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwasili na kusalimiana na viongozi mbalimbali wa serikali katika hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, lililopo eneo la Pongwe nje kidogo ya  jiji la Tanga ambalo linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Bi.Chiku Gallawa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
IMG_1571
IMG_1592
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka saini kitabu cha wageni katika meza kuu. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Gallawa.
IMG_1833
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga leo  kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez,  ambalo linasimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.

IMG_1627
Baadhi ya wanachi wa jiji la Tanga wakimsikiliza mgeni rasmi Mh. Dk. Mohammed Gharib Bilal wakati akisoma hotuba yake.
IMG_1812
Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mh. Dk. Abdallah Kigoda akitoa risala yake wakati wa hafla hiyo ambapo amewaahidi wakazi wa Tanga kufufua viwanda vyote vilivyokufa mkoani humo.
IMG_1794
Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor  Bw. Chris Incheul Chae akizungumza machache na wakazi wa Tanga na kuwaambia kwamba hawatojutia nafasi waliyowapa wawekezaji hao kutoka nchini Korea ya Kusini.
IMG_1644
 Wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi eneo la Viwanda lililopo Pongwe nje kidogo ya mji wa Tanga.
IMG_1770
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru akizungumzia mradi huo ambapo ametoa  kwa Mkoa wa Tanga kuhakikisha wanafikisha miundombinu muhimu kama maji na umeme ili wawekezaji wasije kupata kikwazo wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
IMG_1744
 Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akitoa salamu kwa wananchi ambapo amesema wakazi wa Tanga sio wavivu kama fikra za waliowengi na kusema watachangamkia fursa hiyo kubadilisha maisha yao.
IMG_1727
 Mbunge wa Tanga Mjini, Mh. Injinia Omary Nundu (CCM) akizungumza na wananchi wake na kusema kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake kupitia fursa mbalimbali na kuwataka kutoa ushirkiano kwa wawekezaji hao.
IMG_1805
Aisee tunashukuru sana kwa kutupa nafasi ya kuwekeza nchini kwako…! Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor  Bw. Chris Incheul Chae (kulia)akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru wakati wa hafla hiyo.
IMG_1679
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Gallawa akitoa nasaha zake kwenye halfa kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, lililopo eneo la Pongwe nje kidogo ya  jiji la Tanga ambalo linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.
IMG_1993
Mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akirusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Bi.Chiku Gallawa (kushoto) na Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor  Bw. Chris Incheul Chae ( wa pili kulia).
IMG_1996
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru (kushoto), Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi wakishiriki zoezi la kurusha mchanga.
IMG_1891
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, baada ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi la ujenzi wa viwanda katika eneo hilo wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo jijini Tanga.
IMG_1937
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na kupewa maelezo baadhi ya vifaa kama Solar Cooker, ambavyo ni baadhi ya vitakavyokuwa vikizalishwa katika Viwanda hivyo baada ya kukamilika, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo jijini Tanga.
IMG_2011
Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Bi.Chiku Gallawa akiserebuka na wanakikundi cha uhamasishaji mara baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk. Bilal baada ya kuweka jiwe la msingi.
IMG_2014
 Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akijumuika na wamama wakitanga wakati wakitoa burudani.
IMG_1673
 Washiriki wa Redd’s Miss Tanga 2013 nao walikuwa nu miongoni mwa wageni wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
IMG_1619
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
IMG_1615
IMG_1630
Wananchi wa jijini Tanga wakiwa wamefurika eneo la Pongwe kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika nchi yetu.
IMG_1635
Wana CCM wakionyesha nyuso za furaha na matumaini kwa vizazi vyao vitakavyonufaika na ajira kupitia mradio huo.
IMG_2044
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Korea na baadhi ya viongozi wa Serikali.
IMG_2077
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wawekezaji kutoka nchini Korea.
IMG_2059
Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor  Bw. Chris Incheul Chae akimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa kumshukuru kubariki ujenzi wa viwanda hivyo.
IMG_2027
Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwapungia wananchi wa Tanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi  la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, lililopo eneo la Pongwe nje kidogo ya  jiji la Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa.
IMG_2111
Baadhi ya wakazi wa Tanga wakisoma ramani ya ujenzi wa viwanda hivyo katika eneo Maalum la Pongwe lilipo nje kidogo ya jiji la Tanga.
Na. Mo Blog Team, Tanga.
Jumla ya ajira 2000 zinatarajiwa kuzalishwa katika awamu ya kwanza ya mradi wa ukanda wa viwanda Mkoani Tanga, unaotarajiwa kuanza mwaka huu hadi mwaka 2015.
Akizingumzia mradi huo kwenye eneo la Pongwe nje kidogo ya Mji wa Tanga, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda, amesema mradi huo ambao utatekelezwa na kampuni ya Afrika Future Forum kutoka Korea ya Kusini utazalisha ajira hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa viwanda 20.
Kwa mujibu wa Waziri huyo hadi sasa tayari wawekezaji 17 wameshaonesha nia ya kuja kuwekeza huku viwanda viwili vinatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor Chris Incheul Chae, amesema  mradi huo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 277.
Chae amesema viwanda vitakavyokamilika kwa mwaka huu na kuanza kazi mara moja ni cha vifaa vya ujenzi na kiwanda cha mafuta aina ya petroli ambayo yatauzwa kwa bei ambayo mtanzania wa kawaida ataimudu.
Katika kuhakikisha ajira zinatoka humu humu nchini, amesema watachukua wahitimu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi(VETA) na Chuo Kikuu Huria.
Naye Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumzia ujio wa mradi huo, amesema Serikali itatoa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza mradi huo pamoja na kuwavutia wawekezaji wengine nchini kutimiza azma ya mapinduzi ya viwanda.
Hata hivyo amewataka watendaji kuacha tabia ya kuwazungusha wawekezaji wanapokuja nchini kwa kuweka taratibu zenye urasimu usiokuwa na tija kwa taifa .
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru, ametoa wito kwa Mkoa wa Tanga kuhakikisha wanafikisha miundombinu muhimu kama maji na umeme ili wawekezaji wasije kupata kikwazo wakati wa utekelezaji wa mradi huo.