Monday, 17 June 2013

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI , CCM YAIZIKA RASMI CHADEMA IRINGA


CHAMA cha mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa kimeshinda kwa  kimbunga  uchaguzi mdogo  wa madiwani kata ya Mbalamaziwa wilaya ya Mufindi na kata ya Nga'ang'ange  wilaya ya Kilolo mkoani Iringa dhidi  ya  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema)

Katika  matokeo  hayo ya  uchaguzi ambayo mtandao  huu wa  www.matukiodaima.com umeyapata  kwenye kata ya Ng'ang'ange  wilaya  ya  Kilolo ambayo msimamizi msaidizi  wa uchaguzi huo Esabela  Kamwela ameyatangaza  amesema  kuwa  jumla ya  wapiga kura  walikuwa  919 kati ya  1087 waliojiandikisha kupiga kura.

Alisema  kuwa katika  uchaguzi huo ambao umemalizika katika hali ya utulivu na amani mgombea wa Chadema alikuwa ni Lucas Chaye na  mgombea wa CCM alikuwa ni Namgeleki Yohanas  na  kuwa  wagombea  wote  wamekubali matokeo na  kusaini fomu za  uchaguzi za  tume .

Kamwela  amesema  kuwa katika  uchaguzi huo  jumla ya  kura 16 ndizo zilizoharibika na kura 903 zilipigwa huku  mgombea wa Chadema akianguka  vibaya kwa  kupata  kura 217 na mgombea wa CCM akiimbuka  kidedea kwa kura 686.


Wakati kagtika kata ya Mbalamaziwa  ambako  pia  kulikuwa na mvutano mkubwa wa  uchaguzi kati ya  CCM na Chadema  kiasi cha wafuasi wake  kutambiana kwa  kupigana nguvu wakati wa kufunga kampeni pia  Chadema imepata  pigo  kubwa baada ya  kushindwa  vibaya  dhidi ya CCM.

Mbalamaziwa ambako ni jirani kabisa na kata  ya Nyololo ambayo mwaka  jana mwezi wa tisa mwenyekiti wa  wanahabari mkoa  wa Iringa Daud Mwangosi aliuwawa katika vurugu za Chadema na polisi  pia  Chadema imeonekana  kukataliwa na wananchi  baada ya  mgombea  wake  Ezekiel Mlyuka kuambulia kura 185 pekee huku  mgombea  wa CC Zuberi Nyomolelo akizoa  kura 1426 na kura  26 zikiharibika .

Hata  hivyo  matokeo hayo yamepokelewa kwa  mikono miwili toka kwa wagombea  wote na sasa  inasubiriwa  siku ya  kuapishwa kwa  madiwani hao  wateule.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...