Thursday, 13 June 2013

TANAPA YAKABIDHI TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA

224 b117e
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi Musa Juma kutoka gazeti la Mwananchi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja na laki tano aliyoshinda baada ya kuandika makala nzuri ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tuzo inayoandaliwa na shirika la hifadhi za taifa TANAPA kwa waandishi wa habari wa Televisheni, Redio na Magazeti katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watuzo hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hiltop Hotel ya mjini Iringa, hafla hiyo imefanyika baada ya mkutano wa siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA katika ikiwa na kauli mbiu ya Jukumu la Vyombo vya habari Katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa uliomalizika leo , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA

322 b1878
Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi Mwandishi Albano Midelo wa Gazeti la Dira tuzo aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...