Thursday, 13 June 2013

KAMPENI ZA UCHAGUZI WA UDIWANI ZINAENDELEA ARUSHA

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara,Mh.Mwigulu Nchemba akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Makuyuni wilayani Monduli hii leo tar.12/06/2013.Hapa akisalimiana na wanachama wa CCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara kusikiliza sera za chama chao cha mapinduzi.

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara,Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na moja ya kikundi cha akina mama kata ya Makuyuni wilayani Monduli kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani.

Hii ni sehemu tu ya mamia ya wananchi na wanachama wa CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo wa hadhara.Picha imechukuliwa wakati msafara unapokelewa wa Naibu katibu mkuu Mh.Mwigulu Nchemba

Mh,Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania bara akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kata ya Makuyuni kwenye mkutano wa hadhara hii leo wa kumnadi mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM Ndugu Goodluck Lerunya

Mh;Mwigulu Nchemba(Kushoto) anayefuatia ni mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Makuyuni Ndugu Goodluck Lerunya,Kulia ni Mh:Marry Chitanda Mbunge viti maalumu Tanga wa ambaye pia ni Katibu CCM Mkoa wa Arusha.

Kada wa CCM Ndugu Mtela Mwampamba akihutubia mamia ya wananchi kata ya Makuyuni wilayani Monduli kwenye kampeni za Uchaguzi wa Udiwani.Kada huyu wa CCM amewaomba wananchi wa MAKUYUNI ambao asiliyao kubwa ni kabila la Wamaasai kumchagua mgombea wa CCM kwenye uchaguzi utakao fanyika mapema tar.16/06/2013 siku ya jumapili.Amewasihi wananchi hao kuachana kabisa na siasa za chama cha upinzani kwa sababu vitawaletea vurugu,pia havina dira ya maendeelo.Nanukuu"Vyama vya siasa hasa hicho CHADEMA nashukuru hamkujitokeza kwenye mkutano wao wajana wakaishia kuondoka patupu,Nimekuwa chadema zaidi ya miaka 5 hakuna siku tuliyopanga kuleta maendeleo ndani ya nchi yetu,hivyo vyama ni maarufu kwa kulalamika tu."Hivyo chagueni diwani wa CCM kwamaslahi ya wananchi na jamii yenu.

Kada wa CCM Bi.Juliana Shonza amewaomba wananchi wa MAKUYUNI kumpigia kura kwa wingi mgombea wa CCM kwasbabu ndicho chama chenye kuleta maendeleo kwa wananchi.

Naibu katibuMkuu wa CCM Tanzania bara amewaomba wananchi na wanachama wa CCM kata ya makuyuni kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi bila kuogopa vitisho vyovyote.Mh:Mwigulu Nchemba ameenda mbali zaidi kwa kusema uchaguzi huu wa udiwani si kubadirisha serikali bali ni kuendeleza maendeleo ya serikali iliyopo madarakani.Amesema kumpa kura mgombea wa CCM ndio njia pekee ya kuwaweka wananchi karibu na serikali yao.Pia ilani na sera za CCM zinatekelezeka.Amedai wapinzani hawana sera za kuwaletea maendeleo wananchi,wataishi kulalamika tu.Pia amesema anaamini wmaasai ni kabila lenye ulinzi wa kutosha hivyo watalinda kura siku ya uchaguzi na kuhakikisha mgombea wa CCM anashinda.

"Amani idumishwe siku ya uchaguzi,Swala la ardhi na sehehemu ya malisho ni mambo yanayojadilika,Hivyo nitakuwa nanyi beaga kwa bega,diwani wenu huyu najua atashinda nitakuwa karibu naye katika kutatua matatizo yenu kupitia mbunge wa jimbo hili"

Mgombea wa udiwani kata ya Makuyuni kwa tiketi ya CCM Ndugu Goodluck Lerunya

CCM chama cha maendeleo,chama cha maslahi jamii.Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara akimnadi mgombea wa udiwani kata ya makuyuni kwa tiketi ya CCM Ndugu Goodluck Lerunya.Mh:Mwigulu Nchemba amesema mgombea anakila sababu ya kushinda kwa sababu anauwezo wa kutetea maslahi ya wana Makuyuni

Mkutano Umemalizika,wananchi wanaagana na Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara

CCM ni chama cha nchi nzima na kwa watanzania wote

Naibu katibu Mkuu Mh:mwigulu Nchemba akiondoka viwanja vya kata ya Makuyuni wilayani Monduli jioni hii,hapa akiwapungia mkono wanachama wa CCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni za uchaguzi wa udiwani kata ya Makuyuni

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...