Sunday, 22 September 2013

ABDULRAHMAN KINANA AMJULIA HALI MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI MUSUGULI BUTIAMA, AENDELEA NA ZIARA WILAYANI SERENGETI

1aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu wakati alipomtembelea na kumjulia hali Mjini Butiama leo, wakati akiondoka wilayani humo kuelekea Mugumu Wilaya ya Serengeti kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Jenerali Musuguli alionekana kuwa na bashasha wakati alipomuona Abdulrahman Kinana pengine ni kutokana na utendaji kazi wa katibu mkuu huyo wa CCM,  ambapo alisikika akisema huyu ni kijana wangu huku wakiwa wameshikana mikono wakiingia ndani kwa mazungumzo ya faragha.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MUGUMU SERENGETI2aJenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu akisalimiana na Nimrod Mkono Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi CCM.
3aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Musuguli nyumbani kwake Butiama.4aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo huku Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula akisikiliza kwa makini.5aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Jenerali David Musuguli wakiingia ndani huku wakiwa wameshikana mikono.7aJenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana, na maofisa kadhaa ambao ameongozana nao katika msafara huo, kushoto ni Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono.8aJenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari, kushoto ni Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini.9aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Jenerali David Musuguli wakati alipomtembelea nyumbani kwake leo.  11aJenerali David Musuguli akiagana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi huku wakionekana kufurahia jambo.14aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kata ya Isenye wilaya ya Serengeti15aAkisalimiana na na wana CCM walipokuwa wakimlaki leo 16aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma wakati kikitumbuiza.18Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nata wilayani Serengeti leo.19aWimbo wa taifa 20aWanafunzi wa Shule ya sekondari Nata wakiimba wimbo wa taifa.21aMwalimu Mwema Machage wa Darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Nata akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakati alipokagua shule hiyo22Mwalimu Peter Simon wa shule ya Sekondari ya Nata wilayani Serengeti akielezea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wake somo la sayansi wakati alipotembelea maabara ya shule hiyo.katikati ni mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph23amwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM kuhusu wanafunzi hao wanavyojifunza jinsi ya kutengeneza sabuni katika maabara hiyo ya shule.24aWananchi wakimpungia mkono Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana25Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Isenye29aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mgorole na Mzee Nyangarisi Kumari kuwa mmoja wa wazee wa heshima wa  kimila wa kabila la Kiikoma  tukio hilo limefanyika katika kata ya Bukore.30aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kutawazwa mzee wa heshima wa kabila la Kiikoma katika kijiji cha Bukore wilayani Serengeti

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...