Vijana wa halaiki kutoka shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa wakionyesha umahili wao katika kutoa ujumbe wa Mwenge
Askari wa FFU Iringa wakiwa wamemkamata kijana ambae jina lake bado kufahamika aliyetaka kuvamia mwenge kwa nia mbaya wakati wakimbiza mwenge wakiwa mbioni kukabidhi mwenga kwa Rais Jakaya Kikwete uwanja wa Samora Iringa
Watoto wa halaiki wakiwa wamepumzika
Rais Jakaya Kikwete akiwa amekabidhiwa rasmi mwenge wa Uhuru leo baada ya kuhitimisha mbio zake nchini
Rais Kikwete akiwa ameushika mwenge wa Uhuru leo uwanja wa samora Iringa
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za mwenge kikanda na jumla leo
Rais Jakaya Kikwete akipokea mwenge kwa ajili ya kupiga picha ya pamoja na washindi wa mbio hizo kikanda
Rais Jakaya Kikwete akiwa na viongozi wa dini walioshiriki kumwomba dua baba wa taifa leo
Rais Kikwete akisalimiana na askofu wa Roman Katoliki leo
Wageni mbali mbali wakiwemo mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na rais Kikwete
Wabunge pamoja na katibu mkuu wa CCM Philip Mangula wa kwanza kushoto na Spika wa bunge Anne makinda wa tatu kulia anayefuata ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake nzuri " Mheshimiwa Rais nimeipenda sana hotuba yako leo"
Rais Kikwete akiwa na wabunge wa Chadema Iringa ,mchungaji Peter Msigwa na Chiku Abwao ambao pia walishiriki kilele cha mbio za mwenge
Rais Kikwete akipongezwa na mbunge Chikua Abwao na mbunge Msigwa kushoto
Mbunge Chiku Abwao akipiga picha ya Spika makinda leo uwanja wa samora
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na spika Makinda wa tatu kulia
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya nchuini
Mke wa rais Mama Salima Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na spika Makinda na wakimbiza mwenge Kitaifa leo
Wakuu wa wilaya Gelard Guninita na Venance mwamoto katika picha ya pamoja na mwananchi kulia
Mpiga picha wa TBC akiwa juu ya paa kufuatilia matukio ya kilele cha Mwenge leo
Spika wa bunge Anne Makinda akiwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi
Na matukiodaima.com
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete leo amezima mwenge wa Uhuru huku akiwataka watanzania kuendelea kudumisha amani ,mshikamano na utulivu na kutangaza kiama kwa wale ambao watajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya .
Akiwahotubia watanzania katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa ,rais Kikwete alisema kuwa mbio za mwenge wa uhuru zimekuwa zikiendelea kuwaunganisha watanzania na kuendelea kuibua na kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo nchini .
Hata hivyo alisema wapo baadhi ya watu ambao wameendelea kupinga mwenge wa uhuru ambapo kwa upande wake hawashangai wanaofanya hivyo kwa ni mtazamo wao .
" Wakati leo umma wa watanzania wakiendelea kuushangilia mwenge wa uhuru na hata kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ila wapo baadhi yao ambao hawautakii mema mwenge huu....kama huyu mmoja ambae leo amejionyesha hapa ...sasa sijui mwenge umemkosea nini"
Mbali ya hilo pia Rais Kikwete alisema kuwa serikali yake imejipanga vema kuhakikisha inachukua hatua sitahiki kwa wale wote wanaojihusisha na biashara na utumiaji wa madawa ya kulevya .
Kwani alisema mbali ya kazi kubwa inayofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ila bado baadhi ya watu wameendelea kuifanya kazi hiyo ya dawa za kulevya na kuwataka watanzania kushirikiana na serikali katika kuwafichua wahusika wa dawa za kulevya na serikali itawalinda wale wote wanaotoa taarifa za wahusika wa dawa za kulevya.
Aidha Rais Kikwete alisema kuwa pamoja na kuwa hivi sasa Taifa limekuwa katika utulivu mkubwa wa amani ila bado watanzania wanapaswa kuendelea kuenzi amani ambayo baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere aliiacha na kupitia mwenge wa uhuru watanzania wamekuwa wakiendelea kumuenzi kwa kuyatenda yale ambayo mwenge wa Uhuru umekuwa ukiyabeba.
Rais Kikwete alisema kuwa si vema watanzania kuendelea kugawanywa kwa misingi ya itikadi, dini, rangi ama raslimali kwani iwapo watanzania tutakubali kugawanywa kwa misingi hiyo tutakuwa tunalipeleka taifa pabaya na kila mtanzania anapaswa kuendelea kuenzi amani iliyopo na kuchukia mgawanyiko wa aina yeyote.
Akielezea kuhusu janga la ukimwi alisema kuwa bado tatizo hilo la UKIMWI limeendelea kuwa kubwa katika mkoa wa Njombe ambao unaongoza kwa maambukizi ukifuatiwa na mkoa wa Iringa ambao unashika nafasi ya pili kitaifa kwa UKIMWI hivyo kuwataka wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kuchukua hatua ya kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU na kuendelea kutumia dawa ya kupumbaza virusi vya UKIMWI inayotolewa na serikali na wale ambao hawajaathirika kujilinda wasiathirike .
Katika hatua nyingine Rais Kikwete amewataka watanzania kujiandaa kusherekea mapinduzi ya miaka 50 ya Zanzibar ,kukamilika kwa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania shughuli ambazo zitafanyika mwakani.
Wakati huo huo sherehe hizo za kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru nusuru ziingie doa baada ya kijana mmoja ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja kuwavamia wakimbiza mwenge kitaifa na kutaka kukonya mwenge huo kabla ya kukamatwa na kupokea kipigo kikali mbele ya Rais Kikwete toka kwa askari wa FFU.
Tukio la kijana huyo kutaka kupokonya mwenge huo lilitokea dakika chache baada ya waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangala kumwomba Rais Kikwete kushuka jukwaa kuu na kusongea eneo maalum la kukabidhiwa mwenge kutoka kwa wakimbiza mwenge hao.
Wakati wakimbiza mwenge hao wakisogea huku wakiwa karibu kumfikia Rais Kikwrte kama hatua 10 hivi kijana huyo alichomoko kutoka upande ambao wanahabari walikuwa wamesimama na kuwafuata kwa mbele wakimbiza mwenge hao na kutaka kuupokonya mwenge huo .
Hata hivyo kabla ya kuugusa mwenge huo mmoja kati ya vijana wakimbiza mwenge kitaifa kutoka mkoa wa Iringa alimdaka kijana huo na kumnyanyua juu juu kabla ya askari wa FFU waliokuwepo eneo hilo sanjari na mwenge kumkamata na kumpa kichapo na kumpakia katika gari la polisi na kumpeleka polisi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment