Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali, Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini leo mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
Mgimwa akiungana na wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya Ulanda mchana leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba (kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msamba tavangu (katikati) na mgombea ubunge kupitia CCM, Mgimwa wakicheza walipofika kwenye kampeni katika Kijiji cha Kibebe.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Vijana wakimkaribisha kwa kucheza kijana mwenzao Godfrey Mgimwa katika mkutano huo wa kampeni
Nani zaidi?
Mama mkazi wa Kijiji cha Kibebe, Venanzila Kihaga akiwa ameshika kipeperushi cha Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, alipoteuliwa na wanakijiji kumuombea kimila Mgimwa ashinde uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kalenga Tosamaganga,Kisabugo Mkemwa akitoa mahubiri ya kumuombea Mgimwa (kushoto) ili ashinde uchaguzi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Iringa, Aloyce Mgongolwa akisikiliza kwa makini wakati Nchemba akihutubia katika mkutano huo wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe.
Balozi wa CCM Tawi la Kibebebe, Julius Kihaga akiwa makini kusikiliza hotuba ya Mgimwa
Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gabriel Athuman akinywa maji ya kisima ambayo aliyasifia kuwa ni matamu wakati wa mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Kibebe
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Mgimwa akijinaji katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe leo mchana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Mgimwa.
Aliyewahi kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki kupitia Chadema, na Ofisa wa Chadema Makao Makuu, Mwampamba akielezea jinsi alivyoamua kujiondoa kwenye chama hicho bhaada ya kufanyiwa mabaya na uongozi wa Chadema ambacho alidai hakifai wananchi kujiunga nacho.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment