Monday 24 March 2014

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI KATA YA MBWEWE

1Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kik wete katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya shule ya sekondari ya Changarika kata ya Mbwewe jimboni humo, Ridhiwani Kikwete alishiriki yeye mwenyewe kijenga shule hiyo wakati ya sekondari Changarika akiwa katibu wa uhamasishaji UVCCM taifa na amewaomba wananchi wa kata hiyo kumkopesha imani yao kwake na yeye atawalipa maendeleo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- CHALINZE)3Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Pongwe Kiona kata ya Mbwewe leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo.6mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Juma Pinto Mkurugenzi wa Jambo Concerption na William Malecela kulia.
10Sam wa Ukweli akitumbuiza katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Pongwe Kione.11Msafiri Kafiri tutafika tu japo safari ni ndefu.12Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa kampeni katika kijiji cha Pongwe Kiona.13Shaibu Akwilombe katibu wa CCM mkoa wa Mtwara na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa CCM akunguruma katika mkutano huo.14Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo wa kampeni huku wakiwa wameshikilia picha za mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.16Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wananchi mbalimbali katika mkutano huo.17Vijana wa chipukizi waksoma ngojera yao kumkaribisha Ridhiwani Kikwete katika mkutano huo.18Kikundi cha ngoma aina ya Selo wakati wa mkutano huo.19Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akimuombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia CCM Bw. Ridhiwani Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...