Umoja wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza wasema kwamba Mhe. hotuba ya Rais,Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba ,haikururuga wala kuingilia mchakato wa kupata Katiba Mpya ,bali alitoa maoni na ushauri kama kiongozi wa nchi.
Aidha wajumbe hao wamesema Rais hakuingilia kanuni za bunge hilo zilizopitishwa, hakubadilisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na hakupiga kura kwenye vifungu vya Katiba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa wajumbe hao, Said Nkumba katika mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa Bunge mjini Dodoma.
Nkumba ambaye aliambatana na baadhi ya wajumbe wengine watano , ambapo alisema hotuba hiyo imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano wa Tanzania kwa hoja ili Watanzania wawe nnnnnna fursa pana ya kutafakari na kuamua
Aliongeza kuwa alichokifanya Rais katika hotuba yake ni kama kiongozi mkuu wan chi mwenye hekima na busara na uchungu wa nchi yake na kutambua dhamana aliyopewa na Watanzania wote bila kujali makundi ameelezea faida na hasara za mifumo ya Serikali iliyowasilishwa kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba.
“ Rais katupa moyo na kutuhimiza tumalize kazi haraka na tuifanye kwa weledi huku tukiweka maslahi ya taifa mbele. Hata pale alipotoa maoni na ushauri kuhusu baadhi ya vifungu bado alisisitiza kwamba umamuzi wa mwisho ni wetu sisi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,” alisisitiza.
Nkumba alifafanua kuwa dhana ya kuichambua na kuikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba si kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake. Hivyo msingi mzima wa kutolewa rasimu hiyo ni kwamba wananchi waichambue, kuikosoa ,kuboresha na kuirekebisha na hata ikibidi kuibadilisha na mwisho kuipigia kura.
Alisema rasimu hiyo haikuletwa kama Msahafu wala Bibilia Na ndiyo maana zimewekwa hatua mbili baada ya kazi ya tume kumalizika ,ambazo ni bunge hilo na kura ya maoni ya wananchi.
Aliwataka wajumbe wa bunge hilo kushirikiana ili kuweza kuifanya kazi hiyo.
Wajumbe wa bunge hilo wa Tanzania Kwanza wapo takribani 400 na watatoka katika makundi mbalimbali ,ambaomsimamo wao ni kushawishi kwa hoja na wala hawatalazimisha.
No comments:
Post a Comment