
Naibu Waziri wa Maji Mh. Binilith Mahenge.
Na Immaculate Makilika- Dodoma
Serikali
imemwajiri Mtaalamu Mshauri wa kusanifu miundombinu ya maji katika
mji wa Magu,hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya
Kikwete la kutatua tatizo sugu la maji kwenye eneo hilo mji wa
huo.
Naibu
Waziri wa Maji Mh. Binilith Mahenge alisema hayo alipokuwa akijibu
swali la Dk. Festus Limbu Mbunge wa Magu –CCM lililouliza ,je,
Serikali haioni kuwa haiwatendei haki wananchi wa mji wa Magu kwa
kutotekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais.
Aidha
Naibu huyo alisema kuwa usanifu huo uliohuisisha miji midogo ya Magu
,Nansio,Misungwi,Ngudu,Sengerema,Geita pamoja na jiji la Mwanza,na
ulikamilika mwezi Septemba mwaka 2011.
Usanifu huo uligharimu sh. bilioni 1.1 ambapo gharama ya ujenzi kwa mji wa Magu ilikadiriwa kuwa sh. bilioni 24.
Hata
hivyo Serikali kwa kushirikiana na wafadhili itagharamia ujenzi wa
miradi ya maji ya jiji la Mwanza ,miji ya Misungwi ,Magu ,Lamadi na
usafi wa mazingira kwa miji ya Bukoba na Musoma.
Benki
ya Maendeleo ya Ulaya (EB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD)
watatoa jumla ya Euro milioni 105 sawa na sh. bilioni 214
kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Kabla
ya kuanza ujenzi ,wafadhili waliona wajiridhisha na gharama zaujenzi
kwa kufanya mapitio ya usanifu uliofanyika awali na kujumuisha vijiji
vilivyopo umbali wa kilometa 12 kutoka bomba kuu.
Wataalamu
washauri wanaopendekezwa kufanya mapitio ya usanifu wa miradi hiyo
watawasilisha mapendekezo yao ya kiufundi na kifedha mwanzoni mwa
mwezi June mwaka 2013,alisema Naibu Waziri huyo.
No comments:
Post a Comment