NA MAGREGH KINABO – MAELEZO DODOMA
SERIKALI imewaagiza watendaji na wananchi kupitia kamati za o za afya kuhakikisha misamaha inatolewa kwa wote wanaostahili.
Aidha imesema
kuwa kituo ambacho hakifanyi vizuri katika ukusanyaji na udhibiti wa
matumizi ya fedha zinazotokana kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), viongozi husika wapewe onyo. Baada ya muda
watakaopewa iwapo hakuna mabadiliko zichukuliwe hatua za kinidhamu
ikiwa ni pamoja na kuondolewa madaraka waliyopewa.
Kauli hiyo
ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi
wakati akifungua mkutano wa mkutano mkuu wa mwaka wa waganga wakuu wa
mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na
taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia, wadau wa
maendeleo na washiriki kutoka Tawala za Mkoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI).
Mkutano huo wa siku tatu umefanyik katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper mjini Dodoma.
“Mwongozo wa
Serikali kuhusu sera ya ucahangiajia wa huduma za afya nchini
unajulikana. Lakini kuna vituo ambavyo bado vinaendelea kutoza gharama
za uchangiaji wa huduma ,kwa makundi ya watu ambayo sera inaelekeza
huduma zitolewe bila malipo. Wizara imekuwa ikilamzimika kujibu
malalamiko mengi kuhusu vituo ambavyo havitekelezi maelezo hayo,
Nimeambiwa kuwa
katika ukusanayaji wa fedha zinazotokana na kutoa huduma kwa wanachama
wa NHIF , vituo binafsi vinaongoza kupata fedha nyingi kuliko umaa
pamoja na ukweli kwamba wana wagonjwa wachache wanaohudumia. N aamini
tunajua sababu “alisema Dk. Mwinyi.
Hata hivyo alisema wongozo huo unapitiwa ili uendane na mahitaji ya kisasa.
“Tunajua umuhimu
wa vituo vyetu kuwa fedha za kutosha kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa
wananchi . hivyo sisi viongozi lazima tutumie njia zote halali za
kupata fedha ,pia tuweke usimamizi madhubuti wa kukusanya na kutumia
fedha hizo, endapo hakutakuwa na udhibiti imara uboresahji wa huduma
hautakuwepo hata kama kuna fedha nyingi,” alissitiza.
Alisema kauli
mbiu ya mkutano huo ni ‘Usimamizi Bora wa Utendajia Kazi ndiyo nguzo Kuu
katika utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii’. Hivyo changamoto
nyingi zinazojitokeza katika huduma za afya zinaweza kuondolewa na
usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji kazi wa walio chini.
Dk. Mwinyi
aliongeza kuwa tatizo la upungufu wa watumishi katika vituo vya huduma
za afya bado lipo. Idadi ya watumishi hao waliopo hadio kufikia Aprili
mwaka 2013ni 64,449, ambayo ni asilimia 47 yawanaohitajika katika vituo
hivyo.
Kwa upande
wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dk. Rufaro Chatora
alisema anampongeza waziri huyo kwa kujibu hojan kwa umahiri na
kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.
Aliongeza kuwa
changamoto za kiafya zinazoikabili nchi ya Tanzania, pia kwa nyingine
duniani. Hivyo rasilimali kila siku hazitoshelezi, kinachotakiwa ni
kuendelea kuboresha huduma hizo.
Naye Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo , Regina Kikuli alisema mkutano hu unatoa
fursa ya kujadiliana namna ya kuboresha huduma hizo.
Awali
akiwakarisha wageni hao katika mkutano huo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rehema
Nchimbi alisema mkoa wake umefanikiwa kutekeleza mpango wa chanjo.

No comments:
Post a Comment