Saturday, 1 June 2013

JAPAN YAIKOPESHA TANZANIA BILIONI 54 ILI KUBORESHA KILIMO CHA MPUNGA NCHINI

J2Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini  hati ya makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam  kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.J1Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 54.13 jana jijini Dar es salaam  kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji mpunga hapa nchini. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamaniPSTKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah(kushoto)  akifafanuzi umuhimu wa ujenzi wa miundombinu mipya ya kilimo cha umwagiliaji mpunga  hapa nchini jana jijini Dar es salaam  mara baada ya kusaini hati ya mkopo wa shilingi bilioni 54 kwa ajili ya kuendeleza zao la mpunga. Kulia ni  Balozi wa Japan nchini Masaki Okada. Wilaya 80 zinazolima mpunga zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo kwa kujenga  miundo mbinu mipya na kukarabati ya zamani.
Picha na MAELEZO- Dar es salaam
Na Mwandishi wetu, MAELEZO-Dar es salaam
Japan imeipatia Tanzania imepata mkopo wa shilingi bilioni 54.13 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha umwagiliaji mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Makubaliano hayo yametiwa saini jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah  na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ampapo Wilaya 80 zinazolima mpunga hapa nchini zinatarajiwa kunufaika na mkopo huo.
Akizungumza mara ya kusaini makubaliano hayo Khijjah alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kukarabati miundo mbinu ya zamani ya umwagiliaji na kujenga miundo mbinu mipya ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kupunguza uagizaji wa mchele kutoka nje ya Tanzania Japan ikiwemo badala yake wananchi wajikite katika kuzalisha hapa nchini bila ya kutegemea mvua.
Aliongeza kuwa mpango ni sehemu ya Mkakati wa Serikali wa Kupunguza umaskini kwa wananchi na kukuza uchumi na hivyo kuboresha maisha ya wanachi kwa kuwahakikishia upatikanaji wa chakula cha kutosha.
Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa chini ya mkopo utasaidia kuongeza uzalishaji kutoka tani 3-4 kwa hekta hadi kufikia tani 6 katika mvuno mmoja.
Alimhakikishia Balozi wa Japan kuwa Serikali itahakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa  malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Naye Balozi wa Japan nchini  Masaki Okada alisema kuwa karibu asilimia 75 ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo na hivyo fedha hizo ni muhimu kwa Tanzania katika kutekeleza malengo yake iliyojiwekea katika Kilimo kwanza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...