Na Magreth Kinabo –Maelezo
Umoja wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza wasema kwamba Mhe. hotuba ya Rais,Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba ,haikururuga wala kuingilia mchakato wa kupata Katiba Mpya ,bali alitoa maoni na ushauri kama kiongozi wa nchi.
Aidha wajumbe hao wamesema Rais hakuingilia kanuni za bunge hilo zilizopitishwa, hakubadilisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na hakupiga kura kwenye vifungu vya Katiba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa wajumbe hao, Said Nkumba katika mkutano na waandishi habari uliofanyika kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa Bunge mjini Dodoma.
Nkumba ambaye aliambatana na baadhi ya wajumbe wengine watano , ambapo alisema hotuba hiyo imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano wa Tanzania kwa hoja ili Watanzania wawe nnnnnna fursa pana ya kutafakari na kuamua
“ Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kulazimisha,” alisema Nkumba.